Matthew 26:20-25

20 aIlipofika jioni, Isa alikuwa ameketi mezani pamoja na wale wanafunzi wake kumi na wawili. 21 bNao walipokuwa wakila, Isa akasema, “Amin, nawaambia, mmoja wenu atanisaliti.”

22Wakahuzunika sana, wakaanza kumuuliza mmoja baada ya mwingine, “Je, ni mimi Bwana?”

23 cIsa akawaambia, “Yule aliyechovya mkono wake katika bakuli pamoja nami ndiye atakayenisaliti. 24 dMwana wa Adamu anaenda zake kama vile alivyoandikiwa. Lakini ole wake mtu yule amsalitiye Mwana wa Adamu. Ingekuwa heri kwake mtu huyo kama hangezaliwa!”

25 eKisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, akasema, “Je, ni mimi Rabi?”

Isa akajibu, “Naam, wewe mwenyewe umesema.”

Kuanzishwa Kwa Meza Ya Bwana

(Marko 14:22-26; Luka 22:14-20; 1 Wakorintho 11:23-25)

Copyright information for SwhKC